SIMBA YATINGA FAINALI SASA KUKUTANA NA AZAM FC IJUMAA

Yanga imeendelea kusulubiwa kwenye mashindano ya Mapinduzi Cup baada ya kujikuta ikichezea kichapo kutoka kwa Simba kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili kwa mikwaju ya penati 4-2 kufatia dakika 90 kumalizika bila timu hizo kufungana.

Baada kichapo cha 4-0 kutoka kwa Azam FC, Yanga imeondoshwa kwenye michuano hiyo na kuziacha Simba na Azam zikutane kwenye mchezo wa fainali ambao utachezwa siku ya Ijumaa January 13, 2017 ikiwa ni siku moja baada ya kilele cha Mapinduzi ya Zanzibar.

Golikipa wa Simba Daniel Agyei ndio alikuwa shujaa kwa upande wa Simba hususan kwenye changamoto ya mikwaju ya penati. Agyei ameokoa penati mbili za Deogratius Munishi na Mwinyi Haji huku yeye akifunga penati yake baada ya Mkude kufunga ya kwanza.

Wachezaji wa Simba waliofunga penati: Jonas Mkude, Daniel Agyei, Mzamiru Yassin na Javier Boukungu

Method Manjale ni mchezaji pekee wa Simba aliyekosa penati ambayo iliokolewa na golikipa wa Yanga Deogratius Munishi.

Simon Msuva na Thaban Kamusoko ndio wachezaji pekee wa Yanga waliofunga penati zao huku Deogratius Minish ‘Dida’ na Mwinyi Haji penati zao zilitua kwenye mikono ya golikipa wa Simba Daniel Agyei.


Comments