WAZIRI MKUU AZINDUA SAFARI ZA NDEGE DAR - DODOMA
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amezindua safari za ndege za Shirika la Ndege
Tanzania (ATCL) kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Makao Makuu ya Nchi,
Dodoma.
Akizindua
safari hizo leo amesema safari hizo zitawezesha wafanyabiashara na
wananchi wengine kutoka Dodoma na kwenda katika maeneo mengine kwa
urahisi.
“Tuna
ndege nzuri. Tuzitumie kwenda katika maeneo mengine kwani gharama zake
ni nafuu. Kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam ni sh. 165,000, kwenda na
kurudi ni sh. 299,000,” amesema.
Amesema
ndege nyingine kama hiyo inatarajia kuwasili nchini Juni mwaka huu
jambo ambalo litaongeza idadi ya safari za ndege hizo nchini na maeneo
mengine ya nchi jirani.
Kwa
upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa ATCL. Kapten Richard Shaidi ametumia
fursa hiyo kuipongeza Serikali kwa ujio wa ndege hizo na kwamba hiyo ni
moja ya mikakati ya Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli ya kufufua ATCL.
“Hivi
karibuni tunaanza kwenda nchi jirani. Mwakani tutapata ndege nyingine
kubwa itakajayokuwa inafanya safari za masafa ya kati na ya mbali” amesema.
Aidha,
Mwenyekiti wa Bodi ya ATCL, Bw. Emmanuel Korosso amesema hivi karibuni
shirika hilo linatarajia kuanza safari za kwenda katika miji ya Tabora,
Songea, Mtwara, Mpanda, Mafia na Jiji la Tanga.
Akizungumzia
kuhusu safari za Dodoma amesema zitafanyika mara mbili kwa wiki, siku
ya Ijumaa na Jumatatu. Hata hivyo wanatarajia kuongeza safari hapo
baadae.
Naye
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai ametoa wito kwa wakazi wa Dodoma
kutumia vizuri fursa hiyo ya safari za ndege za ATCL kwa kuwa
utawawezesha kusafiri kwa muda mfupi tofauti na vyombo vingine vya
usafiri.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Jordan Rugimbana ameshukuru kwa
uanzishwaji wa safari hizo kwa kuwa zitarahisisha kutoka katika Makao
Makuu ya nchi na kwenda katika mikoa mingine nchini.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, John
Malecela baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka
uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi
wa safari za ndege za ATCL kati aya viwanja viwili hivyo, Januari 16,
2017.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Spika wa Bunge, Job Ndugai baada
ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa
Julius Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege
za ATCL kati aya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia viongozi na wananchi wa Dodoma baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Januari 16, 2017 ikiwa ni uzinduzi wa Safari za ndege za Shirika hilo kati ya viwanja viwili hivi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisafiri kwa ndege ya Bombardier Q400 ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kutoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere kwenda Dodoma Januari 16, 2017. Alikuwa akizindua safari za ndege za ATCL katika viwanja viwili hivyo. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Leonard Chamuriho.

Comments
Post a Comment