YAHYA JAMMEH KUSALIA MADARAKANI KWA MIEZI MITATU BAADAE

Yahya Jammeh
Bunge la Gambia limeongeza muhula wa Rais wa Gambia Yahya Jammeh ambao unakamilika siku ya Alhamisi kufuatia kushindwa kwake kwenye uchaguzi kwa siku 90.
Bunge pia limeidhinisha uamuzi wa Jammeh wa kutangaza hali ya tahadhari ya siku 90, katika taifa hilo dogo la Afrika Magharibi.
Viongozi wa kanda wametishia kutumia nguvu za kijeshi kumlazimisha bwana Jammeh kuondoka madarakani, ikiwa atakataa kusalimisha mamlaka kwa rais mteule Adama Barrow.
Maelfu ya watalii raia Uingereza na Uholanzi wanaondolewa kutoka Gambia.
Nchi hiyo ni maarufu kwa watalii kutokana na fukwe zake.

Comments