ARSENAL YATINGA ROBO FAINALI FA CUP
Arsenal wamefika robo fainali ya Kombe la FA baada ya kuwalaza Sutton United kupitia mabao ya Lucas Perez na Theo Walcott.
Katika
mechi hiyo iliyochezewa Gander Green Lane,
Wenger alifanya mabadiliko
saba katika kikosi kilichochapwa 5-1 na Bayern Munich mechi ya mkondo wa
kwanza hatua ya 16 bora katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya wiki
iliyopita.
Kikosi chake kilikuwa an nguvu za kutosha kuwazidi
wapinzani hao ambao wamo nafasi 105 chini yao katika orodha ya ustadi wa
klabu Uingereza.
Lucas Perez alifungia Arsenal bao la kwanza
dakika ya 26 naye Theo Walcott akaongeza la pili dakika 10 baada ya
kipindi cha pili kuanza.
Hilo lilikuwa goli lake la 100 kufungia Arsenal.
Ushindi huo ulimpunguzia shinikizo meneja Arsene Wenger.
Arsenal sasa watakutana na Lincoln City katika robofainali.
Lincoln walifika robo fainali kwa kuwalaza Burnley Jumamosi.
Comments
Post a Comment