ASKARI 12 WAPIGWA STOP KAZINI KWA TUHUMA ZA MADAWA YA KULEVYA



Mkuu  wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu amewasimamisha kazi askari 12 ili kupisha uchunguzi kwa tuhuma za kujihusisha na biashara za dawa za kulevya.

 Askari hao ni wale waliokuwa katika orodha aliyoitaja Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati akizungumza na wanahabari hivi karibuni juu ya biashara hiyo.

Mangu aliwaambia wanahabari leo katika Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam, kuwa polisi ndiyo chombo kinachoongoza mapambano dhidi ya biashara ya dawa za kulevya, hivyo askari atakayetuhumiwa lazima achukuliwe hatua.

"Tumeamua kuwasimamisha kazi wote walioguswa moja kwa moja katika sakata hili. Pia polisi itachukua hatua madhubuti  ikiwamo  kuwapeleka mahakamani  wasanii waliotuhumiwa,"amesema Mangu.


Comments