CUF SASA KUDAI TUME HURU YA UCHAGUZI KABLA YA 2020



Chama cha wananchi CUF kimesema kinajipanga kuvishawishi vyama vingine vya siasa na taasisi binafsi kuunganisha nguvu kudai tume huru za uchaguzi kabla ya mwaka 2020.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho zilizopo Vuga, Zanzibar, Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa CUF-Bara, Joram Bashange alisema maandalizi yanaendelea na hivi karibu watatoa tamko.

Bashange alisema wajumbe wa kamati ya utendaji ya chama hicho chini ya Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad katika kikao walichofanya walikubaliana kusukuma suala hilo ili kuhakikisha uchaguzi ujao unakuwa huru na wa haki.

Alisema  ikiundwa tume huru ni wazi itasaidia kufanikisha  uchaguzi ujao na kwamba, mawakala hawatatolewa vituoni, kura zitahesabiwa kwa uhuru na matokeo yatatangazwa kwa mujibu wa sheria.

Pia, alisema walikubaliana mchakato huo uhusishe makundi yote ya kisiasa na kijamii ili kuonyesha umoja wao.


Comments