MCHEZAJI BORA WA AFCON 2017 ATENGEWA DAU NONO HUKO CHINA
Kiungo wa kati wa
Cameroon Christian Bassogog, amejiunga na klabu ya China ya Henan
Jianye, inayoshiriki michuano ya ligi kuu ya Uchina kutoka klabu ya
Aab Fodbold.
Mapema mwezi huu shambuliaji huyo mwenye umri wa
miaka 21 alitajwa kuwa mchezaji bora wa Afcom baada ya Cameroon kupata
ushindi wao wa tano kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya
kombe la Taifa nchini Gabon.
Aab imemuuza Bassogog kwa klabu ya Henan Jianye FC kwa rekodi ya uhamisho kuelekea Aab, klabu hiyo imesema katika taarifa yake.
Bassogog amesema pendekezo la China hangeweza kulikataa.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon alishiriki
mechi zote sita katika Kombe la Mataifa , na kufunga bao katika hatua ya
nusu fainali pale Indomitable Lions walipowachapa Ghana 2-0.
Kwa
sasa anakuwa miongoni mwa wachezaji wa kiafrika kuelekea Uchina , baada
ya mchezaji wa Nigeria John Mikel Obi na Odion Ighalo walipojiunga na
Tiajin Teda na Changchun Yatai mtawalia mwezi uliopita.
Comments
Post a Comment