MOURINHO ASEMA CHELSEA NDIO MABIGWA MSIMU HUU
Meneja wa
Manchester United Jose Mourinho amesema klabu ya Chelsea inaweza
kuangazia michuano ya FA kwani tayari wanajua ni mabingwa wa Ligi ya
Premia.
Vijana hao wa Antonio Conte, ambao watawakaribisha United
Stamford Bridge katika robo fainali Kombe la FA mwezi Machi, wamo mbele
kwa alama nane katika msimamo wa ligi na bado wamesalia na michezo 13.
Chelsea
waliendelea na makali yao kwa kuchapa Wolves 2-0 katika raundi ya tano
Kombe la FA, huku United wakitoka nyuma na kupata ushindi wa magoli 2-1
dhidi ya Blackburn.
''Kombe la FA ni kitu muhimu kwao,'' amesema meneja wa zamani wa Blues, Mourinho.
Chelsea
wanapigiwa upatu kushinda ligi kwa mara ya pili kwa miaka mitatu baada
ya Mourihno kutwaa ubingwa akiwa nao msimu wa 2014-2015.
"Chelsea
wanaweza kuangazia vyema michuano ya FA, kwa fikira zangu kwani ni
mabigwa na hawana michuano mingine inayowatatiza. Kombe la FA ni muhimu
kwao.2
Katika msimu wa kwanza kwa meneja Mourinho uwanjani Old
Trafford, ameongoza klabu hiyo kuwa miongoni mwa timu 32 bora katika
ligi ya Europa, ambapo kwa sasa wamo kifua mbele kwa magoli 3-0 dhidi ya
Saint- Etienne ya Ufaransa .
United wanashikilia nafasi ya sita katika jedwali la ligi ya Premia.
Comments
Post a Comment