POLISI AMUUA MWENZAKE KISHA NAE KUJIPIGA RISASI KISA USHABIKI WA MPIRA
POLISI amemuua mwenzake kwa kumpiga risasi usiku wa kuamkia leo na
yeye amejiua baada kutazama mechi ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kati
ya Manchester City na Monaco.
Kabla ya polisi huyo,
Konstebo Constable Patrick Kihagi kujiua kwa
kujipiga risasi kichwani, alimjeruhi polisi mwingine kwa kumpiga risasi
begani.
Polisi aliyekufa ametajwa kwa jina la Konstebo James Makokha, na kabla ya kifo alikuwa akifanya kazi Jogoo House.
Inadaiwa kuwa Makokha alipigwa risasi wakati akitaka kumaliza ubishani kati ya Kihagi na Ng’etich.
Kabla ya tukio hilo saa saba na nusu usiku kwenye eneo la Tassia,
Nairobi nchini Kenya, polisi hao watatu walikuwa baa wakitazama mpira na
kisha wakaanza kubishana, wakatoka nje.
Mashuhuda wanadai kuwa, walipotoka nje walizidi kubishana, Kihagi
akatoa bastola na kumjeruhi mwenzake, Konstebo Dominic Ng’etich kwa
risasi.
Kihagi alikuwa akifanya kazi katika kituo cha Embakasi, Ng’etich
anafanya kazi kwenye kituo cha polisi kwenye Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Jomo Kenyatta.
Comments
Post a Comment