UMEZIONA CAMERA ZILIZOFUNGWA UWANJA WA TAIFA KUELEKEA MECHI YA SIMBA VS YANGA
Kwa
wale wanaokwenda Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kufanya vurugu
hasa wakati wa mechi ya watani, Yanga na Simba itakaypigwa Jumamosi
ijayo, waahirishe.
Kitengo cha ulinzi uwanjani hapo kimesisitiza kutakuwa na ulinzi mkali pamoja na kamera za ulinzi ambazo ziko tayari kwa kazi.
Hashim
Abdallah ambaye ni mwamuzi lakini ni askari Polisi, amesisitiza wako
imara na kuwaonya weote ambao wanafikiri wanaweza kufanya vurugu ikiwa
ni pamoja na kung’oa viti bila ya kujulikana.
Kamera za kisasa zitatumika kuwanasa kila watakaofanya vurugu na mara moja hatua za kisheria zitachukuliwa.
Katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyowakutanisha watani hao, mashabiki wa Simba wenye jazba waling'oa na kuvunja kiti hasa baada ya Amissi Tambwe kufunga bao upande wa Yanga. Kabla ya kufunga alishika, lakini mwamuzi hakuchukua hatua yoyote na mashabiki hao wakaamua kumaliza hasira zao kwenye viti.
Comments
Post a Comment