WALIORIPOTI KWA MAKONDA KWA TUHUMA ZA MADAWA YA KULEVYA WASOTA RUMANDE

TID

Wema Sepetu


Wakati macho na masikio ya Watanzania wakisubiri kusikia hatma ya wasanii wanaodaiwa kujihusisha na dawa za kulevya, wasanii wanne waliofika Kituo Kikuu cha Polisi bado wanashikiliwa na
jeshi hilo kwa mahojiano zaidi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kuwa bado wasanii hao Wema Sepetu, Dogo Hamidu, Khalid Mohamed TID, na mtangazaji maarufu wa Clouds TV Babuu wa Kitaa bado wanashikiliwa na jeshi  hilo.

“Bado tunawashikilia kwa mahojiano zaidi,” amesema Sirro kwa kifupi.

Wasanii wengine waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambao wanatakiwa kufika kituoni Jumatatu ni Vanessa Mdee, Tunda na watu wengine Halidali Kavila, Amani, Kashozi na Omary Sanga.


Comments