LEMA NJE KWA DHAMANA

Godbless Lema
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo imemuachia kwa dhamana Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema baada ya kukaa mahabusu kwa muda wa miezi minne.


Lema aliyekamatwa mapema mwezi Novemba mwaka jana amekuwa akikwama mara kwa mara kupatiwa dhamana katika kesi inayomkabili ya uchochezi dhidi ya Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Mahakama imemuachia baada ya kutimiza masharti ya dhamana yaliyokuwa yakimtaka kuwa na wadhamini wawili na shilingi milioni 1.

Comments