SUMAYE AJITOA KWENYE BODI YA WAKURUGENZI CRDB
Aliyekuwa
Waziri Mkuu wa serikali ya awamu ya tatu, Frederick Sumaye amejitoa
katika Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB kwa madai kuwa familia yake
inafuatwafuatwa hivyo kuhofia kuwa anaweza kuathiri benki hiyo.
Baada
ya kujitoa kama mmoja wa viongozi wa benki hiyo kubwa nchini, Sumaye
amesema kuwa ataendelea kuwa mwanahisa wa benki hiyo ya biashara.
“Sitaki
msimamo wangu wa kisiasa uhusishwe na benki yetu” alisema Sumaye ambaye
ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya
Pwani.
Sumaye
alisema kuwa huenda majukumu yake ya kisiasa yakambana na akashindwa
kuhudhuria baadhi ya vikao muhimu vya benki hiyo ambavyo ni muhimu kwa
ufanisi na ustawi wa benki.
Akiwa
nje ya mkutano huo Sumaye alisema kuwa, familia yake imekuwa
ikifuatwafuatwa na serikali na kwamba tayari mtoto wake amepokwa shamba.
Serikali
pia alimnyang’anya Sumaye shamba lake lililokuwa Mabwepande kwa madai
hakuliendeleza, huku yeye akisema uamuzi wa yeye kupokwa shamba ulikuwa
ni wa kisiasa. Sumaye alieleza kwamba hakuweza kulima shamba hilo
kutokana na serikali kupiga kilimo jijini Dar es Salaam.
Sumaye
amesema uamuzi wake aliuchukua ili CRDB iweze kuendeshwa na watu
walioko huru mbele ya jamii kuepusha hisa za wafanyabishara wengine
kuathiriwa.
Sumaye anamiliki zaidi ya hisa milioni 7.4 za benki hiyo.
Comments
Post a Comment