AUDIO: RPC WA MWANZA AMEZUNGUMZIA MAUAJI YALIYOTOKEA

Endelea kutembelea blog yetu kuwa wa kwanza kuhabarika kwa maoni na ushauri +255 766 086 039 +255 625 715 167 +255 744 063 802 +255 719 980 891 +255 684 219 786




Mtoto Ester Maxmilian (17) ameelezea vifo vya wazazi wake waliofariki baada ya baba yake kumpiga risasi mama na yeye kujipiga risasi.

Wawili  hao ni Maxmilian Tula (40) aliyejipiga risasi kifuani baada ya kumpiga risasi tatu mkewe Teddy Malulu (38) huku chanzo vifo hivyo kikiwa na utata.
Wanandoa hao wamezaa watoto wawili, Ester na Grace Maxmilian huku mwanamume akidaiwa kuwa watoto wengine wawili Faith na Fero aliozaa na mwanamke mwingine nje ya ndoa.
Akisimulia mkasa huo nyumbani kwao mtaa wa Kanyerere Kata ya Mahina wilayani Nyamagana jijini Mwanza, mtoto huyo amesema ugomvi wa wazazi wake ambao ulidumu kwa takriban saa moja ulianza baada ya mama yake kurudi nyumbani saa 5.00 usiku akiwa amelewa na kumkuta baba yake  ambaye alirejea nyumbani tangu saa 3.00
Hata hivyo amesema baba na mama yake wamekuwa wakigombana lakini siku hiyo ilikuwa tofauti.
“…Sisi tulikuwa chumbani kwetu tumelala na wao wakawa wanazozana na kutufuata chumbani kwetu.”
Amesema kuwa wakati wa majibizano hayo mama alikuwa akitoa maneno machafu kwa baba, kisha wakaondoka kwenda chumbani kwao.
“Ila baba akamwambia mama kuwa wewe kila siku unanifanyia hivi ila leo ni mwisho, baadaye tulisikia mama akiaza kulalamika akidai kuwa utaniua na kuomba msamaha baba anakataa.”
“Baada ya muda tulisikia risasi tatu zimefyetuliwa, tena tukasikia risasi nyingine ya nne ndipo tulipoenda chumbani tulikuta mama anagaragara chumbani akisema mwangalieni baba yenu amejiua kwa risasi na mimi mnipeleke hospitali, alikuwa amepigwa risasi begani, paja na tumboni.” alisema Ester
Mwenyekiti wa mtaa huo, William Ngongo amesema mwanamke huyo alipelekwa hospitali ya rufaa ya Bugando na saa 1.00  asubuhi walipata taarifa kuwa amefariki dunia ila mwanamume alifia palepale tukio hilo ni kwanza kutokea.

Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi amesema chanzo cha tukio hilo kinachunguzwa
Msikilize RPC Ahmed Msangi kwenye link hapo chini
https://www.audiomack.com/song/ukweli-100/ahmed-msangi-azungumzia-mauaji-mwanza 

Comments