BARABARA MBOVU ZASABABISHA VIFO VYA WAJAWAZITO DODOMA

Endelea kutembelea blog yetu kuwa wa kwanza kuhabarika kwa maoni na ushauri +255 766 086 039 +255 625 715 167 +255 744 063 802 +255 719 980 891 +255 684 219 786

 NA SAMWEL ANDREW, DODOMA
Ubovu wa barabara katika kata ya Chahwa, iliyopo manispaa ya Dodoma, unapelekea kutokea kwa vifo vya akina mama wajawazito pindi wanapotakiwa kuwahishwa katika kituo cha kutolea huduma za afya.

Barabara hiyo ambayo ina mashimo makubwa na kuwa finyu kutokana na miti iliyoota katika barabara hiyo inapelekea ugumu kwa wakazi wa kata hiyo hasa wanapohitaji kwenda vjiji jirani.
Akizungumza na Blog hii, Diwani wa kata ya Chahwa, Bwana Sospeter Mazengo, amesema barabara hiyo haijachongwa kwa muda mrefu na imekuwa kero kubwa kwa wakazi wa kata yake.
Mazengo, pia ameitupia lawama halmashauri kutokana na ubovu wa barabara hiyo kwa kushindwa kuchonga kwa muda mrefu na kutokutoa tenda ya ukarabati kwa kampuni nyingine za ujenzi wa barabara.
Aidha, Ubovu wa barabara hiyo, unapelekea wananchi kushindwa kusafirisha mazao yao hali inayorudisha nyuma maendeleo katika kata hiyo.

Comments