BODI YA WADHAMINI CUF KUKATA RUFAA KISUTU
Endelea kutembelea blog yetu kuwa wa kwanza kuhabarika kwa maoni na ushauri +255 766 086 039 +255 625 715 167 +255 744 063 802 +255 719 980 891 +255 684 219 786
Bodi ya
Wadhamini ya Chama cha Wananchi (CUF) kupitia wakili wake, Hashimu Mziray
imewasilisha kusudio la kukata rufaa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Kupinga uamuzi
uliotolewa Mei 21, 2017 na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri wa kuyatupilia
mbali maombi yao waliyoyafungua mahakamani hapo dhidi ya wabunge wawili,
Magdalena Sakaya(Kaliua), Maftah Nachuma(Mtwara Mjini) na wenzao sita.
Walikuwa
wakiomba mahakama hiyo iwazuie kwa muda kujihusisha katika masuala ya uongozi
na kufanya mikutano ya chama.
Akiwasilisha
kusudia la kukata rufaa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mziray alisema
hawakuridhika na uamuzi huo kwa sababu si kweli kuwa CUF haina bodi ya
wadhamini.
Wakili Mziray
alisema CUF ni chama ambacho kipo hai, kina wabunge, madiwani, majengo,
wanachama na hata Msajili wa Vyama vya Siasa hajakifuta.
Alibainisha
kuwa Hakimu Mashauri akulielewa tangazo la Wakala wa Vizazi na Vifo(RITA) hivyo
wanaiomba Mahakama Kuu kutengua uamuzi wake kwa madai kuwa ni batili.
Awali katika
uamuzi uliotolewa na Hakimu Mashauri ambao uliyatupilia mbali maombi ya Bodi
hiyo alizisikiliza pande zote mbili na kuzitolewa uamuzi huo.
Comments
Post a Comment