UPDATE:MUHONGO ATAKIWA KUJITUMBUA MWENYEWE HARAKA IWEZEKANAVYO
Rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli amemtaka waziri wa nishati na
madini Profesa Sospeter Muhongo ajifikirie na bila kuchelewa achukue hatua ya
kuachia madaraka.
Rais magufuli amesema
hayo muda mfupi tu baada ya kupokea taarifa ya kamati ya kuchunguza mchanga wa
madini (makinikia) yanayopatikana maeneo mbalimbali hapa nchini.
Rais pia ameagiza
vyombo vya ulinzi na usalama kuwachunguza na kuwachukulia hatua watendaji
wengine wa wizara ya nishati madini akiwemo kamishna wa madini aliyekuwepo
kipndi cha miaka mine iliyopita.
Comments
Post a Comment