CHADEMA CCM MWENDO MDUNDO WAKUBALIANA JAMBO HILI

Endelea kutembelea blog yetu kuwa wa kwanza kuhabarika kwa maoni na ushauri +255 766 086 039 +255 625 715 167 +255 744 063 802 +255 719 980 891 +255 684 219 786

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Humphrey Polepole amesema kuwa ni ruksa kwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA) kutumia ukumbi wao wa mikutano maarufu kama 'Dodoma Convention Centre'.

Kauli hiyo imetolewa na Polepole kufuatia mazungumzo aliyofanya kwa njia ya simu na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikael Mbowe tarehe 14 Mei 2017 juu ya uwezekano wa chama hicho kutumia ukumbi huo. Polepole amemwambia Mbowe kuwa CCM haioni uzito wa kutoa kibali kwa CHADEMA kutumia ukumbi huo ikiwa watawasilisha maombi rasmi kwa Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana.

Hata hivyo, Polepole amemweleza Mbowe kuwa wataruhusiwa tu kuutumia ukumbi huo ikiwa watakubali masharti ya kutoweka alama za chama chao nje ya ukumbi huo isipokuwa sehemu ya ndani.

Tarehe 27 Mei 2017, CHADEMA watafanya Mkutano wa Kamati Kuu Mjini Dodoma na taarifa iliyotolewa na Msemaji wa chama hicho Boniface Makene haijabainisha ukumbi watakaotumka. Upo uwezekano kuwa Mbowe ametekeleza masharti aliyopewa na huenda mkutano huo utafanyika ndani ya ukumbi wa CCM.

Comments