CHENGE, WEREMA WAWEKWA KIKAANGONI SAKATA LA MCHANGA

Endelea kutembelea blog yetu kuwa wa kwanza kuhabarika kwa maoni na ushauri +255 766 086 039 +255 625 715 167 +255 744 063 802 +255 719 980 891 +255 684 219 786

Mwigulu Nchemba

Waziri   wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amewachana  wanasheria wakuu wa Serikali wastaafu kwa kuwataka waeleze hadharani maslahi walionayo kwenye kampuni za madini zinazosafirisha mchanga nje ya nchi.


Wanasheria hao wakuu wa serikali wastaafu, ni Andrew Chenge na Jaji Frederick Werema na amewataka wamwache  Rais John Magufuli aendelee kulinda rasilimali za umma, zisiliwe na watu wachache.

Mwingulu amesema hayo juzi wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa  na mamia ya wananchi wa Tarafa ya Ndago, jimbo la Iramba.

 Alisema Chenge na Werema kwa nyakati tofauti wakiwa wanasheria wakuu wa Serikali, pamoja na majukumu yao mengine, wameshiriki kusaini  mikataba mikubwa mikubwa, ikiwemo ya makampuni ya kuchimba madini.

 “Kwa akili ya kawaida tu, baadhi ya mikataba mikubwa ikiwemo ya makampuni ya madini, haikuwa sawa… Ndio maana imelalamikiwa kwa muda mrefu,” alifafanua Mwigulu.
 

Comments