DUTERTE ATANGAZA UFILIPINO KUWA YA KIJESHI KWA SIKU 60

Endelea kutembelea blog yetu kuwa wa kwanza kuhabarika kwa maoni na ushauri +255 766 086 039 +255 625 715 167 +255 744 063 802 +255 719 980 891 +255 684 219 786


Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte alionya Jumatano kwamba anafikiria kuweka nchi nzima chini ya sheria ya kijeshi, akisema wapiganaji wa kigaidi wanaweza kuendelea kushambulia zaidi si tu kusini mwa nchi hiyo bali katika maeneo mengine ya nchi.


Duterte alitangaza Jumanne usiku sheria ya kijeshi kwa siku 60 katika kisiwa cha Mindanao na kisiwa cha  majimbo jirani cha Basilan, Sulu na Tawi-Tawi baada ya mapigano kati ya jeshi la serikali na dola la Kiislamu (ISIS) katika maeneo ya Marawi, mji wa mkoa wa Lanao del Sur katika kisiwa cha Mindanao kusini mwa Ufilipino.

Duterte alitoa tamko hilo katika ziara rasmi ya Urusi, ambayo alilazimishwa kuikatisha baada ya vurugu kutokea katika mji wa Marawi Jumanne mchana.

Comments