GARI LA RUVU SHOOTING LILILOBEBA WACHEZAJI LAPATA AJALI

Endelea kutembelea blog yetu kuwa wa kwanza kuhabarika kwa maoni na ushauri +255 766 086 039 +255 625 715 167 +255 744 063 802 +255 719 980 891 +255 684 219 786

Msafara wa Timu ya Ruvu Shooting Umepata Ajali mbele Kidogo ya Singida wakiwa safarini kurejea Dar Es Salaam.


Ruvu Shooting walikuwa njiani wakiokea Shinyanga walipocheza mchezo wao wa kumalizia msimu wa 2016/2017 wa Ligi Kuu soka Tanzania bara dhidi ya Stand United  

Taarifa kutoka kwa mmoja wa wachezaji waliokuwapo zinasema kwamba gari  hilo likiwa katika Mwendo, tairi lilipasuka na kusababisha gari kuhama Njia na kuparamia miti iliyokuwa jirani.
 
Hakuna mtu yoyote aliyeumia sana japo kuna mchezaji mmoja ambaye amepata Majeraha ya kawaida.

Comments