KAMA HUJAPATA BAHATI YA KUISIKIA RIPOTI YA KAMATI YA KUCHUNGUZA MCHANGA WA MADINI NIMEKUWEKEA HAPA ISOME
Endelea kutembelea blog yetu kuwa wa kwanza kuhabarika kwa maoni na ushauri +255 766 086 039 +255 625 715 167 +255 744 063 802 +255 719 980 891 +255 684 219 786
MUHTASARI
TAARIFA
YA KAMATI MAALUM ILIYOUNDWA NA RAIS WA
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JOHN POMBE
MAGUFULI
KUCHUNGUZA MCHANGA ULIO KATIKA MAKONTENA
YENYE
MCHANGA WA MADINI (MAKINIKIA) YALIYOPO KATIKA
MAENEO
MBALIMBALI NCHINI TANZANIA.
Utangulizi
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli
aliteua Kamati maalum ya wajumbe wanane kuchunguza aina na
viwango
vya madini yaliyomo kwenye mchanga wa madini uliomo ndani ya
makontena
yaliyozuiliwa na Serikali kusafirishwa nje ya nchi. Uteuzi huo
ulifanyika
tarehe 29/03/2017. Wajumbe wa Kamati hiyo wana taaluma katika
fani
za jiolojia, kemia, uhandisi kemikali na uhandisi uchenjuaji madini.
Chimbuko
la kufanyika kwa uchunguzi huu ni kutokana na ukweli kuwa
viwango
vya madini yaliyopo kwenye makinikia havijulikani, na hata mikataba
ya
uchenjuaji makinikia haipo wazi. Hali hii inaleta hisia kuwa nchi inaibiwa na
hainufaiki
na uchimbaji wa madini.
Katika
kutekeleza uchunguzi huu, Kamati iliongozwa na Hadidu za Rejea
zilizoridhiwa
na Serikali ambazo ni:
1.
Kufanya uchunguzi kwenye Makinikia yaliyopo Bandari ya Dar es
Salaam,
Bandari Kavu na migodini kwa kupekua na kubaini vitu
vilivyomo
ndani pamoja na kuchukua sampuli za makinikia ili
kuzifanyia
uchunguzi wa kimaabara.
2.
Kufanya uchunguzi wa kimaabara na kubainisha aina, kiasi na
viwango
vya madini yatakayoonekana katika makinikia kisha
kubainisha
thamani ya madini hayo.
3.
Kutumia mitambo ya scanners iliyopo katika Bandari ya Dar es
Salaam
kwa ajili ya kujiridhisha na aina ya shehena zilizomo kwenye
makontena
yenye mchanga wa madini; hii ni pamoja na kubainisha
uwezo
wa scanners hizo kuona vitu vyenye ukubwa na maumbile
tofauti
vilivyomo ndani ya makontena yenye makinikia.
4.
Kuchunguza utendaji wa Wakala wa Serikali wa Ukaguzi Madini
(TMAA)
wa kuchukua sampuli za makinikia, uchunguzi wa madini
kwenye
maabara na utaratibu wa ufungaji wa utepe wa udhibiti (seal)
kwenye
makontena kabla ya kusafirishwa nje ya nchi.
5.
Kamati pale itakapoona inafaa inaweza kuongeza Hadidu za Rejea
katika
kuboresha utekelezaji wa majukumu yake. Aidha, Kamati
itakuwa
na mamlaka ya kumwita mtu yeyote kwa lengo la kupata
taarifa.
Utekelezaji
wa Majukumu
Ili
kutekeleza uchunguzi huu, Kamati ilifanya yafuatayo:
1.
Kuandaa mpango kazi.
2.
Kukusanya nyaraka na taarifa mbalimbali kuhusiana na makontena
yenye
makinikia yaliyozuiliwa na Serikali kusafirishwa nje ya nchi.
3.
Kutembelea maeneo yote yenye makontena yenye shehena za makinikia
ili
kuyachunguza na kuchukua sampuli zake. Maeneo hayo ni Bandari
Hivyo,
thamani ya dhahabu katika makontena 277 yaliyozuiliwa
bandarini
ni kati ya TZS bilioni 676 na bilioni 1,147.
Taarifa
tulizopata kutoka kwa wazalishaji pamoja na Wakala wa
Serikali
wa Ukaguzi Madini (TMAA) zinaonesha kuwa makinikia
yana
wastani wa takriban 200 g/t. Kiwango hiki ni sawa na kilo 4 za
dhababu
kwenye kila kontena. Hivyo, makontena 277 ya makinikia
yaliyozuiliwa
Bandari ya Dar es Salaam na Bandari Kavu yatakuwa na
tani
1.1 za dhahabu. Kiasi hiki cha dhahabu kina thamami ya TZS
bilioni
97.5 (USD 44,320,000). Thamani hii ni ndogo sana
ukilinganisha
na thamani halisi iliyopatikana katika uchunguzi huu ya
kati
ya TZS bilioni 676 na bilioni 1,147. Kutokana na tofauti hii
kubwa
kati ya viwango vya dhahabu vilivyopo kwenye taarifa za
usafirishaji
na vile ambavyo Kamati imevibaini, ni dhahiri kuwa Taifa
linaibiwa
sana kupitia usafirishaji wa makinikia nje ya nchi.
2.
Pamoja na viwango vikubwa vya dhahabu kwenye makinikia, Kamati
ilipima
na kupata viwango vikubwa vya madini ya copper (kiwango
cha
15.09% hadi 33.78%, wastani wa 26%), silver (kiwango cha 202.7
g/t
hadi 351 g/t, wastani wa 305 g/t), sulfur (kiwango cha 16.7% hadi
50.8%,
wastani wa 39.0%) na iron (kiwango cha 13.6% hadi 30.6%,
wastani
wa 27%).
Copper
Wastani
wa kiwango cha copper kilichopatikana ni tani 5.2 na
kiwango
cha juu kilichopimwa ni tani 6.75 kwenye kila kontena lenye
tani
20 za makinikia. Hivyo, kiasi cha wastani wa copper kwenye
makontena
277 ni tani 1,440.4 ambazo thamani yake ni TZS bilioni
17.9
(USD 8,138,260) na kiasi cha juu ni tani 1,871.4 ambazo zina
thamani
ya TZS bilioni 23.3 (USD 10,573,478). Hivyo, thamani ya
copper
katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS
bilioni
17.9 na bilioni 23.3.
Nyaraka
za usafirishaji ambazo Kamati ilizipata kutoka bandarini
zinaonesha
kuwa makinikia yana wastani wa kiwango cha copper cha
20%.
Kiwango hiki ni sawa na tani 4 za copper kwenye kila kontena;
hivyo
makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini yatakuwa na tani 1,108
za
copper. Kiasi hiki cha copper kina thamami ya USD 6,204,800
sawa
na TZS bilioni 13.6. Kwa takwimu hizi, kwa upande wa copper
nako
kuna upotevu mkubwa wa mapato ya taifa ukizingatia kuwa
usafirishaji
wa makinikia nje ya nchi umefanyika kwa muda mrefu.
Silver
Wastani
wa kiwango cha silver kilichopimwa ni 6.1 kg na kiwango
cha
juu ni 7 kg kwa kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, kiasi
cha
wastani wa silver kwenye makontena 277 ni 1,689 kg (tani 1.7)
ambazo
thamani yake ni TZS bilioni 2.1 (USD 937,446); kiasi cha juu
ni
1,939 kg (tani 1.9) ambazo thamani yake ni TZS bilioni 2.4 (USD
1,075,757).
Hivyo, thamani ya silver katika makontena 277
yaliyozuiliwa
bandarini ni kati ya TZS bilioni 2.1 na bilioni 2.4.
Nyaraka
za usafirishaji ambazo Kamati ilizipata kutoka bandarini
zinaonesha
kuwa makinikia yana silver kwa wastani wa takriban 150
g/t.
Kiwango hiki kinamaanisha kuwa kuna 3 kg za silver kwenye kila
kontena
la tani 20 za makinikia. Kwenye makontena 277
yaliyozuiliwa
bandarini, kiasi cha silver kilichopo kwenye nyaraka za
usafirishaji
ni 831 kg. Kiasi hiki cha silver kina thamami ya USD
461,039
sawa na TZS bilioni 1.0. Kwa takwimu hizi, kwa upande wa
silver
nako kuna upotevu mkubwa wa mapato ya taifa.
Sulfur
Wastani
wa sulfur uliopimwa ni tani 7.8 wakati kiwango cha juu
kilikuwa
tani 10.2, kwa kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo,
makontena
277 yaliyozuiliwa bandarini, yatakuwa na wastani wa tani
2,161
za sulfur, ambazo thamani yake ni TZS bilioni 1.4 (USD
648,130);
na kiasi cha juu ni tani 2,825.4 ambazo zina thamani ya TZS
bilioni
1.9 (USD 844,296). Hivyo, thamani ya sulfur katika makontena
277
yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 1.4 na bilioni 4.9.
Thamani
hii ya sulfur ni kubwa ukizingatia kuwa haijawahi kutumika
kukokotoa
mrabaha katika mauzo ya makinikia.
Iron
Wastani
wa iron uliopimwa ni tani 5.4 wakati kiwango cha juu
kilikuwa
tani 6.1, kwa kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo,
makontena
277 yaliyozuiliwa bandarini yatakuwa na wastani wa tani
1,496
za iron, ambazo thamani yake ni TZS bilioni 2.3 (USD
1,047,060);
na kiasi cha juu ni tani 1,695 ambazo zina thamani ya TZS
bilioni
2.6 (USD 1,186,668). Hivyo, thamani ya iron katika
makontena
277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 2.3 na
bilioni
2.6. Kama ilivyo kwa sulfur, thamani hii ya iron ni kubwa
ukizingatia
kuwa haijawahi kutumika kukokotoa mrabaha katika
mauzo
ya makinikia. Hali hii inazidi kuonesha jinsi gani nchi yetu
isivyofaidika
na uuzwaji wa makinikia nje ya nchi.
3.
Uchunguzi pia umeonesha kuwepo kwa madini mkakati (strategic
metals)
ambayo kwa sasa hivi yanahitajika sana duniani na yana
thamani
kubwa sambamba na thamani ya dhahabu. Madini hayo ni:
iridium,
rhodium, ytterbium, beryllium, tantalum na lithium.
Iridium
Wastani
wa iridium uliopimwa ni 6.4 kg wakati kiwango cha juu ni
13.75
kg kwa kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, makontena
277
yaliyozuiliwa bandarini, yatakuwa na wastani wa 1,773 kg za
iridium,
ambazo thamani yake ni TZS bilioni 108 (USD 48,876,096);
wakati
kiasi cha juu ni 3,808.8 kg ambazo thamani yake ni TZS
bilioni
231.0 (USD 105,007, 238). Hivyo, thamani ya iridium katika
makontena
277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 108 na
bilioni
231.
Rhodium
Wastani
wa rhodium uliopimwa ni 0.034 kg wakati kiwango cha juu
ni
0.078 kg kwa kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo,
makontena
277 yaliyozuiliwa bandarini yatakuwa na wastani wa 9.4
kg
za rhodium, ambazo thamani yake ni TZS bilioni 0.7 (USD
300,731);
wakati kiasi cha juu ni 21.6 kg ambazo thamani yake ni
TZS
bilioni 1.5 (USD 689,912). Hivyo, thamani ya rhodium katika
makontena
277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 0.7 na
bilioni
1.5.
Ytterbium
Ytterbium
ilipatikana kuwa na wastani wa 3.7 kg na kiwango cha juu
kilikuwa
4.9 kg kwa kila kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo,
makontena
277 yaliyozuiliwa bandarini yatakuwa na wastani wa
1024.9
kg za ytterbium, ambazo thamani yake ni TZS bilioni 12.4
(USD
5,636,950); wakati kiasi cha juu ni 1,357.3 kg ambazo thamani
yake
ni TZS bilioni 16.4 (USD 7,465,150). Hivyo, thamani ya
ytterbium
katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya
TZS
bilioni 12.4 na bilioni 16.4.
Beryllium
Wastani
wa kiasi cha beryllium kilichopimwa ni 19.4 kg na kiasi cha
juu
kilikuwa 26.9 kg kwa kila kontena lenye tani 20 za makinikia.
Hivyo,
wastani wa beryllium kwenye makontena 277 ni tani 5.4 zenye
thamani
ya TZS bilioni 6.0 (USD 2,719,143); na kiwango cha juu
kilichopimwa
katika makontena 277 ni tani 7.5 ambazo thamani yake
ni
TZS bilioni 8.3 (USD 3,770,358). Hivyo, thamani ya beryllium
katika
makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni
6.0
na bilioni 8.3.
Tantalum
Tantalum
ilipatikana kuwa na wastani wa 11.7 kg na kiwango cha juu
kilikuwa
17.3 kg kwa kila kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo,
makontena
277 yaliyozuiliwa bandarini yatakuwa na wastani wa
3240.9
kg za tantalum, ambazo thamani yake ni TZS bilioni 1.9 (USD
855,598);
wakati kiasi cha juu ni 4,792 kg ambazo thamani yake ni
TZS
bilioni 2.8 (USD 1,265,114). Hivyo, thamani ya tantalum katika
makontena
277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 1.9 na
bilioni
2.8.
Lithium
Wastani
wa kiasi cha lithium kilichopimwa ni 21.5 kg na kiasi cha juu
kilikuwa
29.8 kg kwa kila kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo,
wastani
wa lithium kwenye makontena 277 ni 5,955.5 kg zenye
thamani
ya TZS bilioni 1.0 (USD 468,698); na kiwango cha juu
kilichopimwa
katika makontena 277 ni 8,254.6 kg ambazo thamani
yake
ni TZS bilioni 1.4 (USD 649,637). Hivyo, thamani ya lithium
katika
makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni
1.0
na bilioni 1.4.
Jumla
ya thamani ya aina zote za Metali Mkakati katika makontena 277
yaliyoko
bandarini ni kati ya TZS bilioni 129.5 na bilioni 261.5. Pamoja na
kuwa
na thamani kubwa, metali hizi hazikuwa zinajulikana kuwemo
kwenye
makinikia na hivyo hazijawahi kujumuishwa kwenye kukokotoa
mrabaha
na hivyo kuikosesha Serikali mapato makubwa kwa kipindi chote
cha
biashara ya makinikia.
4.
Kwa ujumla thamani ya metali/madini yote katika makinikia kwenye
makontena
277 yaliyozuiliwa bandarini, ni TZS bilioni 829.4 kwa
kutumia
viwango vya wastani na TZS bilioni 1,438.8 kwa kutumia
viwango
vya juu. Kwa kuwa viwango hivi vya thamani havitumiki
kukadiria
mapato ya Serikali, ni wazi kuwa kuna upotevu mkubwa
sana
wa mapato kwa nchi yetu.
5.
Thamani zote za madini kwenye makinikia yaliyo ndani ya makontena
zilizoainishwa
hapo juu, zimepatikana kwa kutumia uzito wa wastani
wa
tani 20 za makinikia kwenye kila kontena. Hata hivyo, katika
kupima
uzito wa makinikia ndani ya makontena, kuna makontena
kadhaa
yaliyokuwa na uzito zaidi ya tani 20 za makinikia, kwa mfano
makontena
yenye namba CAIU 2461301, TCLU 0701267, MRKU
6880530
na MSKU 4280570 yalikuwa na makinikia yenye uzito wa
tani
23.1; 22.9; 22.7 na 22.2, kwa mtiririko huo. Hivyo basi, ongezeko
hili
la uzito linaongeza thamani ya makinikia na hivyo kuongeza
upotevu
zaidi wa mapato ya Serikali.
6.
Pamoja na kuchunguza makinikia, Kamati pia ilichunguza shehena ya
mbale
za copper ndani ya makontena matano (5) yaliyozuiliwa
bandarini.
Sampuli za mbale hizo zilipatikana kuwa na viwango vya
dhahabu
hadi kufikia 38.3 g/t, viwango ambavyo havikuoneshwa
kwenye
ripoti ya upimaji wa kimaabara wa TMAA, na hivyo
kutotumika
katika kukokotoa malipo ya mrabaha Serikalini.
7.
Uchunguzi wa Kamati kuhusu utendaji wa Wakala wa Serikali wa
Ukaguzi
Madini (TMAA) umebaini kuwa Wakala haufungi utepe wa
udhibiti
mara baada ya kuchukua sampuli kwenye makontena.
Ufungaji
wa utepe wa udhibiti hufanyika baada ya siku kadhaa katika
hatua
za mwisho za usafirishaji wa makontena. Hali hii inatoa mianya
ya
kufanyika udanganyifu wa kiasi, viwango na thamani ya makinikia
baada
ya uchukuzi wa sampuli.
8.
Kamati pia ilichunguza uwezo wa scanner inayotumika bandarini
kukagua
vilivyomo ndani ya makontena. Katika uchunguzi huu,
ilibainika
kuwa scanner hiyo haina uwezo wa kuonesha vitu
vilivyomo
ndani ya makinikia bali inaonesha umbo tu la shehena ya
makinikia.
Mapendekezo
Kutokana
na matokeo ya uchunguzi huu yanayoonesha upotevu mkubwa wa
mapato
ya Serikali kupitia usafirishaji wa makinikia nje ya nchi, ni muhimu
Serikali
kuchukua hatua zifuatazo haraka iwezekanavyo:
1.
Serikali iendelee kusitisha usafirishaji mchanga wa madini “makinikia”
nje
ya nchi mpaka pale mrabaha stahiki utakapolipwa Serikalini kwa
kuzingatia
thamani halisi ya makinikia kama ilivyoainishwa kwenye
uchunguzi
huu.
2.
Serikali ihakikishe kuwa ujenzi wa smelters nchini unafanyika haraka ili
makinikia
yote yachenjuliwe nchini. Hii itawezesha madini yote
yaliyomo
kwenye makinikia kufahamika na kutozwa mrabaha halisi.
3.
TMAA inatakiwa kufunga tepe za udhibiti kwenye makontena mara tu
baada
ya kuchukua sampuli ili kudhibiti udanganyifu unaoweza kutokea
baada
ya uchukuzi wa sampuli.
4.
TMAA ipime metali zote ambazo zipo kwenye makinikia na kutumia
metali
zenye thamani katika kukokotoa kiwango halisi cha mrabaha.
5.
Kutokana na uwepo wa madini mbalimbali yenye viwango tofauti
kwenye
mbale, TMAA ipime viwango vya dhahabu na metali nyingine
muhimu
katika mbale zote zinazosafirishwa nje ya nchi, bila kujali
kilichooneshwa
kwenye andiko la msafirishaji wa mbale husika. Aidha,
Wizara
ya Nishati na Madini ibainishe tabia za mbale (aina za madini na
viwango
vyake) zilizomo kwenye vyanzo mbalimbali nchini.
6.
Serikali ijumuishe metali zote zenye thamani katika kukokotoa mrabaha
wa
makinikia na mbale za madini mbalimbali.
7.
Serikali iwachukulie hatua watendaji wa TMAA na Wizara Mama
kutokana
na kutosimamia vyema tathmini ya viwango halisi vya
madini/metali
mbalimbali vilivyopo katika makinikia na mbale za madini
mengine;
viwango ambavyo hutumika katika kukokotoa mrabaha.
8.
Serikali ifanye uchunguzi wa kushtukiza kwa kadri itakavyowezekana
katika
udhibiti wa uzalishaji na usafirishaji wa madini nje ya nchi ili
kujiridhisha
kuwa taratibu zilizowekwa kisheria zinatumika ipasavyo.
9.
Uchunguzi zaidi ufanywe na wataalam wa mionzi kwenye scanner
zinazotumika
bandarini ili kubaini aina au mfumo sahihi wa scanner
unaofaa
katika kuchunguza mizigo yenye tabia (properties) kama za
makinikia
na mbale za madini mbalimbali.
SHUKRANI
Kwanza
kabisa, Kamati kwa heshma kubwa inapenda kutoa shukrani kwako
wewe
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe
Joseph
Magufuli, kwa kuwa na imani nasi na kututeua kutekeleza jukumu hili
muhimu
la kuchunguza aina na viwango mbalimbali vya madini katika
makinikia
ili kuweza kuondokana na upotevu mkubwa wa pato la taifa kupitia
biashara
ya makinikia yanayosafirishwa nje ya nchi. Ni matumaini yetu kuwa
matokeo
ya uchunguzi huu yatasaidia Serikali kupitia sekta ya madini katika
kuchangia
pato la taifa na kukuza uchumi wa nchi yetu.
Kamati
pia inatoa shukrani za dhati kwa Katibu Mkuu Kiongozi na wasaidizi
wake
wote kwa misaada na ushirikiano wao uliowezesha Kamati kutekeleza
majukumu
yake vizuri.
Aidha,
Kamati inatambua na kuthamini michango iliyotolewa na taasisi
mbalimbali
zikiwemo Vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini, Wakala wa
Jiolojia
Tanzania, Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Mamlaka ya Bandari
Tanzania,
Mamlaka ya Mapato Tanzania, Wakala wa Ukaguzi wa Madini
Tanzania,
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Kiislam
Morogoro.
Mheshimiwa
Rais, kwa heshma kubwa sasa nachukua fursa hii kwa niaba ya
Kamati,
kukukabidhi nakala sita za Ripoti kamili ya uchunguzi huu.
Ninakuomba
uzipokee.
Pia
ninaomba nikukabidhi kifurushi chenye nyaraka zote ambazo Kamati
ilizikusanya
kutoka kwenye taasisi za Serikali zinazohusika katika kusimamia
na
kudhibiti usafirishaji wa makinika nje ya nchi, pamoja na nyaraka kutoka
kwa
wadau mbalimbali wanaohusika katika biashara ya makinikia.
Aidha,
nichukue fursa hii kukufahamisha kwamba sampuli zote za makinikia na
mbale
za copper zilizochukuliwa na Kamati na kufanyiwa uchunguzi wa
kimaabara,
zimehifadhiwa ndani ya kontena moja ambalo liko mahali salama
chini
ya uangalizi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Serikali. Kwa heshma
kubwa
ninaomba nikukabidhi funguo za kontena lililohifadhi sampuli hizo.
Ninaomba
kuwasilisha.
Comments
Post a Comment