MADIWANI DODOMA WAPONGEZA KUFUTWA KWA CDA

Endelea kutembelea blog yetu kuwa wa kwanza kuhabarika kwa maoni na ushauri +255 766 086 039 +255 625 715 167 +255 744 063 802 +255 719 980 891 +255 684 219 786



 NA SAMWEL ANDREW, DODOMA
Madiwani Halmashauri ya manispaa ya Dodoma, kwa pamoja wamewaondoa hofu wananchi wa manispaa kwa kuwaahidi kupima ardhi bila upendeleo.

Madiwani hao, wameyasema hayo katika kikao cha dharura kilichoitishwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma kwa lengo la kumpongeza rais kwa kuifuta iliyokuwa mamlaka ya ustawishaji makao makuu CDA.
Katika kikao hicho mbali ya madiwani hao kumpongeza rais, wamewahakikishia wananchi wa manispaa ya Dodoma kuwa watatenda haki katika kazi yao waliyopewa japo ina ugumu.
Nae, mkurugenzi wa manispaa ya Dodoma, Bwana Godwin Kunambi, amesema wao kama halmashauri wanalo jukumu zito kutokana na eneo ambalo bado halijapimwa ni kubwa na kuwataka wananchi kuwapa ushirikiano pindi watakapoanza majukumu hayo.
 

Comments