MKURUGENZI ACACIA APINGANA NA KAMATI YA RAIS MAGUFULI
Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya ACACIA
Brad Gordon ametoa tamko la kupinga ripoti ya utafiti wa Mchanga wa
Madini (Makinikia) iliyowasilishwa na kamati iliyoongozwa na Prof.
Mruma Ikulu leo.
Brad anasema kila kontena lina dhahabu isiyozidi 4Kg na
kwamba taarifa zilizotolewa na kamati hiyo si za kweli kwasababu wao
wanatumia maabara yenye sifa za kimataifa ya SGS katika kupima
kiwango cha madini kilichomo kwenye mchanga huo.
Anasema kiwango cha madini kinachosemwa na Tume ni mara 10 ya kiwango halisi kilichomo kwenye mchanga huo.
Kuhusu aina nyingine za madini zinazo semekana kupatikana
katika mchanga huo Brad anasema Serikali imekuwa ikilipwa mrabaha wa
4% kutokana na madini hayo (yale yanayouzika)
Anasema kama kweli taarifa na takwimu zilizotolewa na
Tume hiyo ya Magufuli zingekuwa na Ukweli basi Buzwagi na Bulyanhulu
ndio ingekuwa migodi inayoongoza kwa uzalishaji wa Madini ya Dhahabu
duniani.
Comments
Post a Comment