PAKISTAN KUCHUKUA HATUA KUDHIBITI NDEGE ZAKE KUBEBA MADAWA YA KULEVYA

Endelea kutembelea blog yetu kuwa wa kwanza kuhabarika kwa maoni na ushauri +255 766 086 039 +255 625 715 167 +255 744 063 802 +255 719 980 891 +255 684 219 786


Shirika la ndege la serikali nchini Pakistan, linasema kuwa linachukua hatua kuhakikisha kuwa ndege zake hazitumiwi kubeba madawa ya kelevya baada ya dawa ya heroin, kupatikana kwenye ndege zake mbili zinazofanya safari kuenda mjini London.

Tarehe 15 mwezi huu wa Mei, maafisa wa mipaka wa Uingereza walikamata ndege iliyokuwa ikitokea mjini Islamabad ilipowasili uwanja wa Heathrow mjini London na kuikagua kwa saa kadhaa.
Shirika la kukabiliana na uhalifu nchini Uingereza baadaye lilisema kuwa kiwango fulani cha heroin kilipatikana kimefichwa katika sehemu tofauti za ndege hiyo.
Kuna madai kuwa utawala nchini Uingereza ulichukua hatua hiyo kutokana na taarifa ulizopokea kutoka Pakistan.

Comments