POLE POLE, SHAKA WANGURUMA DAR WAMESEMA HAYA

Endelea kutembelea blog yetu kuwa wa kwanza kuhabarika kwa maoni na ushauri +255 766 086 039 +255 625 715 167 +255 744 063 802 +255 719 980 891 +255 684 219 786


Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) umeitaka serikali kupitia upya mikataba yote ya madini ili kubaini kama ina manufaa na maslahi kwa umma.

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka ameyasema  hayo wakati sherehe za kumpongeza Rais John Magufuli kwa kubaini madudu kupitia kamati aliyoiunda kuchunguza mchanga wa madini.
Shaka amesema UVCCM inaunga mkono jitihada hizo kwa sababu ndivyo inavyoelekezwa kwenye ilani ya CCM ambayo anaisimamia.
Mbali na  pongezi hizo Shaka amesema  ipo haja kwa Rais Magufuli kuwaweka pembeni wasaidizi wake ambao bado wanaonekana kuwa na kigugumizi katika kuwatumikia wananchi.
"Hatuko tayari na hatutakubali kushuhudia tena Tanzania ikirejea katika zama za kiza kinene cha ukwapuaji mali, ulaji na wizi wa mali za umma."
"Tunaishauri Serikali iendelee na mikakati yake ya kuhakikisha, ukwapuaji,ubabaishaji, wizi na ufisadi wa mali za serikali vinakomeshwa mara moja,"amesema Shaka.
KATIKA TAARIFA NYINGINE
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amekemea vikali mauaji yanayotokea mkoani Pwani.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa leo, Alhamisi   Polepole amesema kuwa kama CCM wanataka kuona mauaji hayo yanaendelea kukemewa zaidi.
Polepole ameonyesha  masikitiko yake kwa vyama vya upinzani kukaa kimya badala ya kuungana kama Taifa kukemea mauaji ya watendaji wa CCM yanayoendelea mkoani Pwani.
"Kuungana kwenye ruzuku, hapana vyama vinapaswa kuwa na umoja katika masuala mbalimbali ikiwamo mauaji hayo," amesema Polepole.

Comments