POLISI SHINYANGA WATEKELEZA AGIZO LA RC
Endelea kutembelea blog yetu kuwa wa kwanza kuhabarika kwa maoni na ushauri +255 766 086 039 +255 625 715 167 +255 744 063 802 +255 719 980 891 +255 684 219 786
AWALI
Jeshi la
Polisi limeuzingira mgodi wa Bulyanhulu baada ya Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga, Zainab Tellaack kuzuiwa kuingia katika mgodi huo alikokwenda kukagua
iwapo uzalishaji unaendelea bila kuwepo kwa Maofisa wa Wakala wa Ukaguzi wa
Madini nchini (TMAA).
Jeshi hilo
limefanya hivyo baada ya Tellack kuagiza kuimarisha ulinzi katika eneo lote la
mgodi huo kuhakikisha hakuna mtu anyetoka wala kuingia.
Mapema leo,
Mkuu huyo wa mkoa alitembelea mgodi mwingine wa Buzwagi ambao pia unamilikiwa
na kampuni ya Acacia kama ulivyo ule wa Bulyanhulu.
Katika mgodi
wa Buzwagi, Tellack na msafara wake waliruhusiwa kuingia na kishuhudia shughuli
za uchimbaji ukiwa umeshitishwa kwa kukosekana maofisa wa TMAA walioondoka mara
baada ya Rais Magufuli kutangaza kuvunja bodi na kutengua uteuzi wa watendaji
wakuu wa wakala hiyo.
Msafara wa
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Tellack umezuiwa kuingia katika mgodi wa
dhahabu wa Bulyanhulu alikokwenda kukagua iwapo uzalishaji unaendelea bila
kuwepo kwa Maofisa wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini(TMAA).
Maofisa hao
waliondoka mara baada ya ripoti ya uchunguzi wa mchanga wa dhahabu kupokelewa
na Rais John Magufuli.
Akizungumza
kwa njia ya simu jioni hii, Tellack anayefanya ziara ya kikazi wilayani Kahama
amesema ameagiza jeshi la polisi kuimarisha ulinzi katika eneo lote la mgodi
huo kuhakikisha hakuna mtu anyetoka wala kuingia.
Mapema leo,
mkuu huyo wa mkoa alitembelea mgodi mwingine wa Buzwagi ambao pia unamilikiwa
na kampuni ya Acacia kama ulivyo ule wa Bulyanhulu.
Katika mgodi
wa Buzwagi, Tellack na msafara wake waliruhusiwa kuingia na kishuhudia shughuli
za uchimbaji ukiwa umeshitishwa kwa kukosekana maofisa wa TMAA walioondoka mara
baada ya Rais Magufuli kutangaza kuvunja bodi na kutengua uteuzi wa watendaji
wakuu wa wakala hiyo.
Comments
Post a Comment