SABABU ZA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA KUZUIWA KUINGIA BULYANHULU HIZI HAPA
Endelea kutembelea blog yetu kuwa wa kwanza kuhabarika kwa maoni na ushauri +255 766 086 039 +255 625 715 167 +255 744 063 802 +255 719 980 891 +255 684 219 786
Meneja Ufanisi na
Maendeleo ya Jamii wa mgodi wa Bulyanhulu, Elias Kastila amesema
kilichosababisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Terrack na msafara wake
kushindwa kuingia ndani ya mgodi huo ni mfumo wa ulinzi unaotegeshwa muda
maalumu usioweza kubadilika hadi muda huo ufike.
Kastila amesema isingewezekana msafara huo kuingia mgodini kwa sababu
mtambo huo maalumu wa ulinzi ulikuwa umetegeshwa kufunguka saa 12.00 asubuhi ya
leo, Ijumaa.
Kwa misingi hiyo, Kastila amesema hakukuwa na namna nyingine ya kufungua mlango wa kuingilia mgodini, labda kulipua kwa bomu au baruti.
Akizungumzia uamuzi wa Mkuu wa Mkoa kuweka ulinzi wa polisi kuzuia mtu kuingia wala kutoka mgodini, Kastila amesema huo umetokana lengo la kujiridhisha hakuna tu labda kuna njama za kutorosha mali, jambo alilosema uongozi wa mgodi hauwezi kufanya kwa sababu hakuna kitu cha kutorosha wala kuficha kutokana na shughuli zote kufanyika kwa uwazi na utaratibu unaoruhusiwa kisheria.
Kwa misingi hiyo, iwapo uongozi wa Serikali mkoani Shinyanga utataka kutembelea na kukagua shughuli mgodini hapo kama ilivyofanya kwa mgodi wa Buzwagi, basi ulipaswa kwenda eneo hilo kuanzia saa 12.00 asubuhi ya leo.

Comments
Post a Comment