SITA WACHOMWA KISU ZANZIBAR WANNE SIO WATANZANIA
Endelea kutembelea blog yetu kuwa wa kwanza kuhabarika kwa maoni na ushauri +255 766 086 039 +255 625 715 167 +255 744 063 802 +255 719 980 891 +255 684 219 786
Watu sita
wakiwemo wanne raia wageni kutoka nje ya Tanzania wamejeruhiwa vibaya kwa
kuchomwa na kisu usiku wa kuamkia leo katika mgahawa wa Lukman Mkunazi Mjini
Zanzibar.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Hassan Nassir Ali alizungumza na
waandishi wa habari jana ofisini kwake leo amesema kuwa tukio hilo limetokea
saa 1:20 usiku wa kuamkia leo.
Kamanda huyo
amesema kuwa mtuhumiwa aliyetenda tukio hilo ambaye jina lake
halijatambulika ila kwa sura anafahamika, anakisiwa kuwa na umri wa miaka
(25) ambapo hadi wakati huu bado hajapatikana.
Amesema kuwa
kwa mujibu wa uchunguzi wao wa awali wamebaini kuwa mtuhumiwa huyo amefika
katika mgahawa huo na kuwachoma watu watatu ambao walifika mgahawani hapo
kwa ajili ya kujipatia chakula.
Aliwataja
waliojeruhiwa kuwa ni Mauget Gerarol (66) raia wa Ufaransa ambae amejeruhiwa
pembeni ya jicho lake la kulia, Jennifer Wolf (24) raia wa Ujerumani
aliejeruhiwa katika sehemu yake ya kichwa na Anna Catharina(20) raia wa
Ujerumani aliejeruhiwa kichwani.
Kamanda huyo
alisema baada ya mtuhumiwa huyo kuwachoma visu watu hao alikimbia na akiwa
njiani umbali wa mita 60 kutoka eneo la tukio la awali njiani alikutana na
kijana wengine waitwao Hassan Abdallah mkazi wa Kiponda (24) na raia wa
Canada, Liying Liang na kuwajeruhi kwa kuwachoma kisu mdomoni na shavuni.
Alisema pamoja
na kuwachoma watu hao lakini walifanikiwa kuwachoma visu Sajad Hussein
(55) ambapo majeruhi hao wote walikimbizwa hospitalli ya Tasakhtaa Global
iliyopo Majestic kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Alisema
kuwa majeruhi hao wote walipatiwa matibabu na kuruhusiwa lakini Mauget
Gerarol raia wa ufaransa bado amelazwa hospitalini hapo na anaendelea kupatiwa
matibabu.
Comments
Post a Comment