TFDA: NOVIDA HAINA SUMU YA VIRUSI VYA EBOLA
Endelea kutembelea blog yetu kuwa wa kwanza kuhabarika kwa maoni na ushauri +255 766 086 039 +255 625 715 167 +255 744 063 802 +255 719 980 891 +255 684 219 786
Mamlaka
ya Chakula na madawa (TFDA) imewataka wananchi kupuuza taarifa ambazo zimekuwa
zikisambazwa kwa nyakati tofauti kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna
soda aina ya ‘Novida’ kutoka nchini Nigeria zimeingizwa nchini kinyemela na zina
sumu ya virusi vya Ebola na tayari zimesababisha vifo vya watu 180 nchini humo.
Taarifa
ya Mamlaka hiyo iliyotolewa mwishoni mwa wiki iliyopita ikiwa ni mwendelezo wa
taarifa yake ya awali iliyotolewa mwezi Aprili 2017 inabainisha kuwa taarifa
zinazosambazwa za kuingizwa soda zenye sumu ya Ebola haina ukweli na inapaswa
kupuuzwa.
Kwenye
taarifa hiyo, TFDA imeeleza kuwa inatambua uwepo wa soda ziitwazo Schweppes
Novida zinazozalishwa na viwanda vya Coca-Cola Kwanza,Bonite na Nyanza Bottlers
na soda hizo zinazalishwa kwa kuzingatia mifumo bora ya uzalishaji na zinakidhi
vigezo vya usalama na ubora.
‘’Kama
ilivyo kwa bidhaa nyingize za chakula,vipodozi,vifaa vya tiba na
vitendashi,soda za Schweppes Novida ambazo zimesajiliwa na TFDA zimekuwa
zikifuatiliwa katika soko kupitia mifumo liyopo ya udhibiti ili kujiridhisha
kuwa zinaendelea kukidhi vigezo vya usalama na ubora kwa lengo la kulinda afya
ya mlaji’’inabainisha sehemu ya taarifa ya TFDA .
Soda
aina ya Schweppes Novida kwa hapa nchini ilizinduliwa mwaka 2013,
inatengenezwa na kusambazwa na viwanda vya Coca-Cola vilivyopo katika mikoa ya
Dar es Salaam,Mwanza,Mbeya na Kilimanjaro.Soda hizi zinazopendwa na wateja
zinatengenezwa kwa ujazo wa ml 300 na ml 500 zipo za aina ya Mandarin Cooler
zenye ladha murua ya machenza na Pineapple Breeze zenye ladha ya Nanasi.
Comments
Post a Comment