VITA MPYA: GWAJIMA NA BUSHIRI WA AFRIKA YA KUSINI
Endelea kutembelea blog yetu kuwa wa kwanza kuhabarika kwa maoni na ushauri +255 766 086 039 +255 625 715 167 +255 744 063 802 +255 719 980 891 +255 684 219 786
Kumeibuka mvutano mkali kati ya Askofu wa kanisa la ufufuo na uzima Josephat Gwajima wa Tanzania na Nabii Shepherd Bushir wa kanisa la ECG raia kutoka Malawi ambaye shughuli zake anafanyia nchini Afrika ya Kusini kwa kile kinachoelezwa kupishana kauli kwa watumishi hao.
Kwenye moja ya ibada yake nabii Bushiri ameonekana kulaumu kile anachodai kuwa askofu Gwajima anamshambulia madhabauni wakati yeye amesaidia kuiokoa Tanzania na tetemeko la ardhi lililotokea Kagera Septemba 2016, ameongeza kwa kusema kuwa hajui kama askofu Gwajima nia askofu au nani.
Katika video hiyo ambayo imeanza kusambaa wiki hii kwenye mitandao ya kijamii hasa Youtube nabii huyo ambaye pia ana makanisa yake hapa nchini ameongeza kwa kusema kuwa anawaonea huruma washirika wa kanisa la Gwajima kwa kuwa wanadanganywa.
Ameongeza kwa kusema kuwa askofu Gwajima anamuonea wivu kwa kuwa huduma yake inakuwa kwa hiyo anataka kumgombanisha na serikali ya Tanzania ili achukiwe huku akimuonya kuwa akiendelea na tabia hiyo ya kumsema vibaya siku zake zinahesabika.
Leo katika ibada ya jumapili akiwa kanisani kwake askofu Gwajima amesema hakuna mtu ambaye anaweza kujua kifo chake na hatakufa hadi pale atakapotimiza lile lililomleta duniani.
Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima |
Kwenye moja ya ibada yake nabii Bushiri ameonekana kulaumu kile anachodai kuwa askofu Gwajima anamshambulia madhabauni wakati yeye amesaidia kuiokoa Tanzania na tetemeko la ardhi lililotokea Kagera Septemba 2016, ameongeza kwa kusema kuwa hajui kama askofu Gwajima nia askofu au nani.
Katika video hiyo ambayo imeanza kusambaa wiki hii kwenye mitandao ya kijamii hasa Youtube nabii huyo ambaye pia ana makanisa yake hapa nchini ameongeza kwa kusema kuwa anawaonea huruma washirika wa kanisa la Gwajima kwa kuwa wanadanganywa.
Nabii Shepherd Bushir wa ECG |
Leo katika ibada ya jumapili akiwa kanisani kwake askofu Gwajima amesema hakuna mtu ambaye anaweza kujua kifo chake na hatakufa hadi pale atakapotimiza lile lililomleta duniani.
Comments
Post a Comment