WAMILIKI WA VITUO VYA LUNINGA NCHINI KUCHONGEWA KWA SERIKALI HASA TBC

Endelea kutembelea blog yetu kuwa wa kwanza kuhabarika kwa maoni na ushauri +255 766 086 039 +255 625 715 167 +255 744 063 802 +255 719 980 891 +255 684 219 786


Viziwi wameitaka Serikali kuvisimamia vyombo vya utangazaji kuweka wakalimani wa lugha za alama ili waweze kufahamu mambo yanayoendelea nchini.

Akizungumza leo, Jumatano Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania (Chavita),Nidros Mlawa amesema viziwi ni walipakodi kama ilivyo kwa wananchi wengine hivyo wana haki ya kupata taarifa.
"Tunabaguliwa wakati sisi pia ni walipakodi, televisheni hata ya Taifa haina wakalimani wa lugha hatujui nchi inaenda vipi,"amesema.
Amesema wakati umefika kwa wamiliki wa vituo vya utangazaji kuanza kutoa huduma hiyo kama ambavyo kanuni za utangazaji zinavyotaka waweke wakalimali

Comments