WANAFUNZI WAKUTWA NA MISOKOTO 59 YA BANGI KILIMANJARO
Endelea kutembelea blog yetu kuwa wa kwanza kuhabarika kwa maoni na ushauri +255 766 086 039 +255 625 715 167 +255 744 063 802 +255 719 980 891 +255 684 219 786
Watu wawili
wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti huku jeshi la polisi
mkoani Kilimanjaro linawashikilia wanafunzi wa Shule ya Msingi Msamadi iliyopo
wilayani Hai kwa kukatatwa na bangi misokoto 59.
Kamanda wa
polisi mkoani Kilimanjaro Hamisi Issah alisema Mei 28, mwaka huu, majira ya saa
10:30 Kijiji cha Kyengia wilayani Siha mwananmke mmoja Ephrata Masaki(53),
alipigwa na shoti ya umeme wakati akianua nguo.
Alisema nguo
hizo zilikuwa zimeanikwa kwenye waya uliokuwa umegusana na waya wa umeme
nyumbani kwake na kwamba waya huo ulikuwa umechubuka na kusababisha kifo chake.
Alisema Mei
28, mwaka huu, majira ya saa 12:00 jioni, Kata ya Soweto mwanamke mmoja
aliyefahamika kwa jina la Sadia Kamote(39), mkazi wa Sanya juu, aligundua
kufariki kwa mtoto wake wa darasa la kwanza.
Alisema
mwanafunzi huyo aliyejulikana kwa jina la Selemani Said(8) ni wa Shule ya
Msingi Kilingi alifariki baada ya kuteleza kutoka kwenye jiwe na kusombwa na
maji katika mto Karanga katika daraja la Mangia Shirimatunda.
“Mwanafunzi
huyo alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu huku wenzake aliokuwa akiogelea
nao katika mto huo wenzake watatu kunusulika kifo,”alisema Kamanda Issah.
Alisema mwili
wa marehemu Masaki umehifadhiwa katika hospitali ya Kibong’oto kwa taratibu za
mazishi huku mwili wa mtoto huyo umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa
wa Mawenzi.
Katika tukio
lingine Mei 28, mwaka huu, majira ya saa 10:30 katika kijiji cha kwa
Sadala jeshi hilo liliwakamata wanafunzi wanne wakiwa na begi dogo jeusi na
baada ya kuwapekuwa walikutwa na bangi.
“Tulipowahoji
watoto hao walisema walipewa mzigo huo na mama aliyejulikana kwa jina la
Francisca Limo(43) kwa lengo la kwenda kuuza na tayari tumeshawakamata watuhumiwa
kwa mahojiano zaidi,”Kamanda Issah.
Comments
Post a Comment