IGP Sirro afanya mabadiliko kwenye jeshi la polisi

Endelea kutembelea blog yetu kuwa wa kwanza kuhabarika kwa maoni na ushauri +255 766 086 039 +255 625 715 167 +255 744 063 802 +255 719 980 891 +255 684 219 786


IGP Simon Sirro
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amefanya mabadiliko ndani ya jeshi hilo.

Katika mabadiliko hayo, Kamanda Sirro amemteua aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni, Suzan Kaganda kuwa Mkuu wa Kitengo cha Mafao na Fidia Makao Makuu ya Polisi.
Taarifa iliyotolewa leo Jumanne, Julai 18 na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa, imeeleza kuwa nafasi ya Kaganda imechukuliwa na Kamishna Murilo Jumanne.
Kabla ya hapo, Kamanda Jumanne Murilo Jumanne alikuwa Kamanda wa Polisi, mkoa wa Shinyanga.
Nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Jumanne Murilo Jumanne, Shinyanga, imechukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi, Simon Sylverius ambaye alikuwa Ofisa Mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Mara.
Taarifa hiyo imesema, mabadiliko hayo ni ya kawaida yanayotokea ndani ya Jeshi la Polisi ili kuongeza ufanisi na utendaji wa kazi.

Comments