Vipodozi haramu, vyakula vyenye sumu vyakamatwa Songea
Endelea kutembelea blog yetu kuwa wa kwanza kuhabarika kwa maoni na ushauri +255 766 086 039 +255 625 715 167 +255 744 063 802 +255 719 980 891 +255 684 219 786
Idara ya Afya katika
Manispaa ya Songea imefanikiwa kukamata vipodozi na vyakula vyenye sumu vikiwa
na thamani ya zaidi sh.milioni mbili.
Afisa Habari wa
Manispaa hiyo Albano Midelo amesema vipodozi hivyo vimekamatwa katika kipindi
cha kuanzia Aprili hadi Juni mwaka huu katika ukaguzi endelevu ambao unafanywa
na Idara hiyo.
Amevitaja baadhi ya
vipodozi vyenye sumu ambavyo vimekamatwa kuwa ni actif plus, betasol, broze,
cocoderm, carolight, carotone, citrolight,clairmen,cocopulp,corton,diproson na epiderm.
Vipodozi vingine ni,extralair,jaribu,lemonvate
na mekako, miki, Montclair, movate, Naomi, oranvategel, perfect, princes, rapid,
sabuni protex,seven mirackes, toplemon, whiteplus, dodo, teint, superclair,greeting,14
days, dermotyl, natural,gold touch,coco dermbetacort,extral white, fomura avas,
lemon cream na diva maxmum.
Midelo amesema katika
ukaguzi huo pia vimenaswa vipodozi halali ambavyo vimemalizika muda wake vyenye
thamani ya zaidi ya sh.500,000.Vipodozi vilivyomalizika muda wake ni skin
soft,pure glycerine,royal touch,u&me na mambo fresh.
Katika kipindi hicho
Idara hiyo pia imekamata vyakula vilivyokuwa vinauzwa wakati muda wake
umekwisha vyenye thamani ya zaidi ya sh.300,000.
Comments
Post a Comment