Wananchi Masumuni- Mbinga watakiwa kuchangia maendeleo

Endelea kutembelea blog yetu kuwa wa kwanza kuhabarika kwa maoni na ushauri +255 766 086 039 +255 625 715 167 +255 744 063 802 +255 719 980 891 +255 684 219 786

 Na Sholastika Fute MBINGA

Jumla  ya shilingi  milioni mbili laki saba na elfu hamsini na tatu zimepatikana katika kata ya masumuni  wilayani MBINGA  mkoani  RUVUMA  kwa  kipindi cha miezi mitatu.


Haya yameainishwa  na afisa mtendaji  wa kata hiyo MARIA MWAKIPOKILE  katika mkutano uliofanyika  mwishoni  mwa wiki hii wakati akitoa taarifa ya mapato na matumizi na kusema kuwa  katika kiasi cha fedha  iliyopatikana  milioni mbili laki moja  na elfu mbili  mia tano  imetumika katika matumizi  mbalimbali ikiwemo ujenzi wa zahanati ya kata  hiyo.

Sambamba na hayo  ameomba wananchi kutoa michango kwa hiari na kwa wakati ili kuharakisha kuleta  maendeleo ya katika kata hiyo.

INGIA KWENYE LINKI HAPO CHINI KUMSIKILIZA
https://www.audiomack.com/song/ukweli-100/maria-mwakipokile 

Comments